Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Februari 24, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaji Abubakar Zuberi Bin Ally aliyewasili jijini humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Katika ziara hiyo, Mufti anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa ofisi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza pamoja na uzinduzi wa kanzi data za madrasa, hatua inayolenga kuimarisha utendaji na usimamizi wa taasisi za Kiislamu.
Akizungumza katika kikao hicho, RC Mtanda amemshukuru Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke kwa ushirikiano mzuri anaoutoa kwa Serikali, akisisitiza kuwa mashirikiano kati ya viongozi wa dini na Serikali ni nguzo muhimu ya maendeleo ya mkoa.
Kwa upande wake, Mufti amempongeza Sheikh wa Mkoa kwa mshikamano anaouonesha kwa Serikali, akisema umoja huo ni mfano wa kuigwa katika kujenga taifa lenye maadili na heshima.
Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa dini na waumini kuendelea kuiombea nchi, mkoa na viongozi wa kitaifa pamoja na wa kimkoa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.
Mufti pia amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi, akibainisha kuwa misingi hiyo ndiyo chachu ya maendeleo endelevu.
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
