TAMASHA KUBWA LA INJILI KUFANYIKA MWANZA.HAPPY MBUYA

 

Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Happy Mbuya, anatarajiwa kufanya Tamasha kubwa la Injili la kihistoria itakayofanyika tarehe 20/02/2026 katika Kanisa la ICRC Nsumba, Mwanza Kuazia Saa 12 jioni nakuendelea. Ibada hii inalenga kuwakutanisha waumini, wapenda sifa na waabudu kutoka maeneo mbalimbali.


Tukio hili litapambwa na uwepo wa waimbaji wengi wa Injili waliobarikiwa, akiwemo Obby Alpha,Agness Nkugwe,lydia agapith,Victor tumaint Efrazia mgoye Tumaini njole,Bahati simwiche pamoja na waimbaji wengine wengi watakaotumia sauti zao kama chombo cha kuleta faraja, uponyaji na uamsho wa kiroho kwa watu wa Mungu. Kupitia nyimbo za sifa na kuabudu, waumini watapata nafasi ya kumkaribia Mungu kwa uhuru, shukrani na unyenyekevu.

Zaidi ya hayo, 



Ibada hii si tukio la kawaida, bali ni muda maalum wa kukutana na Mungu, kusahau mizigo ya maisha, kuponywa mioyo iliyochoka, na kufanywa upya rohoni. Ni mwaliko kwa kila mmoja vijana, wazee, familia na waumini wote kujitokeza kwa wingi na kushiriki baraka ambazo Mungu ameandaa kwa ajili ya watu wake.

BOFYA HAPA CHINI KUSIKILIZA NYIMBO ZA HAPPY MBUYA




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post