MAGU YAANZA RASMI BIMA YA AFYA KWA WOTE: WANANCHI 11,021 WA KAYA MASIKINI KUNUFAIKA BURE


 NIPE TITLE NZURI YA MTANDAONO KWA HII TAARIFA ' Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jubilate Lawuo amezindua rasmi uhakiki, usajili na utoaji wa kadi za bima ya afya kwa wote wilayani humo ambapo katika awamu ya kwanza zaidi ya wananchi 11,021 wa kaya masikini wanatarajiwa kupatiwa bima hizo bure.


Hatua hiyo inalenga kutekeleza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kampeni zake za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 ambapo aliahidi kwamba ndani ya siku 100 baada ya kuchaguliwa atahakikisha mpango huo wa bima ya afya kwa wote unaanza kutekelezwa.


Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kipeja - kata ya Kandawe - tarafa ya Itumbili - wilayani Magu, DC Lawuo amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanza kutoa kadi za bima ya afya kwa walengwa, ikiwemo wanufaika wa TASAF na wananchi wenye kipato duni.


Mhasibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Mwanza, Francis Marwa amesema tangu zoezi hilo lianze tarehe 23 Februari mwaka huu wilayani Magu, wameshasajili kaya 250 zenye wanufaika zaidi ya 930 katika kata ya hiyo ya Kandawe.


Awali Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Magu, Eusebius Chanjali amesema amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Magu kuwa halmashauri imejipanga kutoa huduma za matibabu kwa ukamilifu ikiwamo utoaji wa dawa ambao umezidi kuimairika sambamba na huduma nyingine za uchunguzi.

TAZAMA HAPA CHINI



Post a Comment (0)
Previous Post Next Post