Kongamano la Tiba ya Familia kuja na mbinu bora za kuimarisha huduma ya afya ya msingi

 


Kongamano la Tiba ya Familia linafanyika leo, Januari 29, 2026, mkoani Morogoro likiwa na lengo la kujadili mbinu bora za kuimarisha huduma ya afya ya msingi kuelekea utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote pamoja na kuboresha utoaji wa huduma jumuishi, uratibu wa huduma na huduma zinazozingatia jamii.


Kongamano hilo limeambatana na kikao kazi kilichowakutanisha Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT), pamoja na Vyuo Vikuu vya Afya na Sayansi Shirikishi vikiwemo MUHAS, Aga Khan University, KCMC University na Kairuki University, ambao ni wadau wakuu wa mafunzo ya Tiba ya Familia nchini.



Aidha, kongamano hilo limewakutanisha wadau wa afya kutoka nchi kadhaa zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Ethiopia, Afrika Kusini, Kanada na Marekani, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kikanda na kimataifa katika kuimarisha mifumo ya afya nchini Tanzania.






Post a Comment (0)
Previous Post Next Post