Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia
uwanja wa KMC, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya
kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyainishwa kwenye
masharti ya
Kanuni ya Leseni za Klabu.
Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani
zitalazimika
kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao
utakapofunguliwa
baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.
TFF inazikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya
viwanja.
%20limeufungia%20uwanja%20wa%20KMC,%20Dar%20es%20Salaam%20kutumika%20kw%20(1).jpg)