WANANCHI WA MKOA WA MWANZA MJITOKEZE KWENYE ZOEZI LA UANDIKISHAJI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU.MH MTANDA

 


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh.Said Mtanda.Amewahamasisha wananchi wote wa mkoa wa mwanza kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Mpiga kura ambalo litatumika katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa hivi karibuni

Amesikika hii leo Julai 05.2024 kupitia Kipindi cha Mchakamchaka Kinachoruka Jembe fm Radio Amesisitiza wananwachi wote kujitokeza kwa wingi na pia kujiandikisha ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi wa Kumi na moja (Novemba) 2024

Aidha Ameongezea kusema kuwa kuanzia Traehe 21 hadi 27 mwezi wa Nane kutakua na zoezi kubwa la wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu kwa ajili ya Uchaguzi mkuu utakao fanyika Hapo mwakani

Zaidi karibu kumsikiliza kupitia hii link hapa chini


Na Maria Makanza

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post