Mahakama ya Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro imemuhukumu miaka 30 Jela Nassoro Ally (48) Mkulima na Mkazi wa Msowelo Wilaya ya Kilosa Mkoa Morogoro kwa kosa la Kulawiti.
Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 13, 2023 kwa mtoto mwenye umri wa miaka 4 na kukamatwa na Jeshi la Polisi siku inayofuata akiwa katika harakati za kutoroka kijijini hapo.
Hukumu hiyo ilisomwa na Mh. Joctan Luswelo katika Mahakama ya Wilaya Kilosa Julai 2, 2024.
