Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Tanzania, CP Awadhi Juma Haji, Machi 18,2024 ameshiriki katika Maadhimisho ya sita ya Siku ya Wadau wa Uvuvi Kanda ya Ziwa ambayo yamefanyika katika Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara .
Kamishna Awadhi amesema kuwa, kiwango cha matukio ya uhalifu yanayofanyika ndani ya ziwa Victoria kwa kipindi cha miezi sita kimeshuka hii ni kutokana na operesheni za mara kwa mara zinazofanyika ndani ya ziwa hilo sambamba na ushirikiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na wadau wa uvuvi.
Kamishna Awadhi pia amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wavuvi ambao sio waaminifu wanaotengeneza matukio kwa kuiba mafuta, kuuza samaki na kusingizia kuwa wametekwa na kutoa taarifa za uongo kwa mamlaka husika, kuacha tabia hiyo mara moja.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Khalfan Haule ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara amepongeza vikao vya mara kwa mara vinavyofanywa na wadau wa sekta ya uvuvi ambavyo ndiyo vimekuwa chachu ya kupuguza uvuvi haramu na matukio ya uvamizi ndani ya ziwa victoria
By Pascal Kadushi



