Waendesha Pikipiki maarufu kama bodaboda wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa kwani ni kinyume cha sheria za usalama barabarani lakini pia hupunguza umakini wa kumudu chombo na kuweza kusababisha ajali.
Hayo yamesemwa Marchi 14, 2024 na Polisi Kata ya Luegu wilaya ya Namtumbo Mkoni Ruvuma Mkaguzi Msaidi wa Polisi Dastani Salamba alipokutana na bodaboda hao kwa lengo la kutoa elimu ya ushirikishwaji wa jamii, utii wa sheria bila shuruti pamoja na elimu ya usalama barabarani.
Aidha Mkaguzi Salamba aliwaasa bodaboda hao kuanzisha kikundi cha bodaboda cha Kata ya Luegu ili kuweza kusaidiana pindi wapatapo matatizo sambamba na kukumbushana kufuata sheria n alama za usalama barabarani ili kujilinda wenyewe dhidi ya ajali pamoja na watumiaji wengine wa barabara.
Vilevile, Mkaguzi Dastan ametoa onyo kali kwa baadhi ya bodaboda wanaodhaniwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha tabia hiyo mara moja badala yake wakawe mabolozi wa kupinga vitendo hivyo vya kihalifu katika jamii sambamba na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
Pia, alihitimisha kikao hicho kwa kuwasisitiza bodaboda hao kushirikiana na jamii kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao ili kudhibiti vitendo vya kihalifu katika jamii na wananchi kuendelea kufanya shughuli za kujipatia kipato kwa
