MHE.MKUU WA WILAYA YA ILEMELA HASSAN MASALA KUANZA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 

                                                        Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Masala


Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mwalimu Hassan Masala Anategemea kuanza kusikiliza kero za wananchi wa wilaya yake,ya Ilemela,Lengo nikutatua kero mbalimbali za wananchi.Atazungukia Kata kadhaa za wilaya hiyo akianza na kata ya Buswelu siku ya Jumatano ya Tarehe 28/02/2024 kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni.


Baada ya kata ya Buswelu ataelekea Kata ya Kiseke itakua ni Alhamis ya  Tarehe 29/02/2024 kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni na Ijumaa ya Tarehe 01/03/2024 kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni atakua Kata ya Kirumba


Ziara yake itaendelea Jumanne ya 05/03/2024 kwa Kata ya Kawekamo kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni.


Jumatano ya tarehe 06/03/2024 ataendelea na ziara kwa kata ya Buzuruga kuanzia saa 4:00 hadi saa 12:00 jioni na kumaliza kwa kata ya Nyamhongolo siku ya Alhamisi ya tarehe 07/03/2024 kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 12 jioni



Mhe Hassan Masala atakua na viongozi mbalimbali kutoka katika Tasisi za Umma,Wakuu wa Idara Halmashauri na Mkurugenzi


Wananchi wote wanakaribishwa kujitokeza ili kutatuliwa kero zao 

Imetolewa na Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilemela

By Pasacal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post