MHE.DKT.TULIA AMKABIDHI NYUMBA MLEAMVU ALIYEMUHAIDI

 

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amezindua na kumkabidhi nyumba aliyomkarabatia Bw. Hosea Kalemale Mkazi wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya ambaye ni mlemavu wa macho leo tarehe 23 Februari, 2024.

Dkt. Tulia amemkabidhi Hosea nyumba hiyo yenye vyumba viwili vya kulala, sebule pamoja na choo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa siku kadhaa mara baada ya kuombwa hitaji hilo.








Post a Comment (0)
Previous Post Next Post