Njombe Yapewa Heshima ya Kuandaa Mei Mosi Kitaifa 2026

 

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe Anthony Mtaka, ametangaza kuwa mkoa huo utakuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa mwaka 2026.

Mhe. Mtaka ametoa taarifa hiyo leo februari 20,2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

“Mkoa umepokea kwa heshima kubwa nafasi hiyo na kutoa rai kwa wananchi wa Njombe kuitumia kama fursa ya kiuchumi kwa kufanya biashara mbalimbali, akibainisha kuwa zaidi ya wageni 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo”, alisema Mhe. Mtaka




Aidha, Mhe. Mtaka amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira katika maeneo yao ili mkoa uwe katika hali nzuri ya kupokea wageni.
Kwa upande wake, Rais wa TUCTA, Ndugu.Tumaini Nyamhokya, amesema wamepokea barua rasmi kutoka Serikalini kuthibitisha kuwa maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa mwaka 2026 yatafanyika Njombe, na kwamba ujio wao ni kwa ajili ya kutangaza rasmi taarifa hiyo.

Ndugu.Nyamhokya amewahimiza wakazi wa Njombe kujiandaa kwa kuboresha huduma mbalimbali, ikiwemo huduma za chakula na malazi, ili kunufaika na fursa zitakazotokana na uwepo wa wageni wengi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post