WANAFUNZI WA DIT MWANZA WAHIMIZWA KUSHIRIKI KULINDA AMANI

 

Wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT), Tawi la Mwanza, wametakiwa kutofumbia macho vitendo vya uhalifu, kuripoti ukatili wa kijinsia na kushiriki kikamilifu katika kulinda amani.

Kauli hiyo imetolewa na ASP Pili Saburi, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nyamagana, pamoja na SGT Raymond Pius, wakati wakiwapa elimu wanafunzi wa chuo hicho kilichopo Sabasaba, Ilemela, Mwanza.

Aidha, wanafunzi wamehimizwa kuwa mabalozi wa usalama, wakitumia maarifa waliyopewa kuelimisha wenzao na jamii inayowazunguka, ili kuendeleza amani na usalama katika mazingira yao.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post