Nyota wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Peter Manyika amefariki Dunia leo asubuhi, Januari 26, 2026, alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya St. Monica Jijini Dar es Salaam.
Kifo chake kimethibitishwa na mwanaye, Peter Manyika Jr., aliyesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, huku msiba ukiendelea nyumbani kwao Mbezi.
Mbali na kuwa mchezaji, enzi za uhai wake Manyika aliwahi pia kuwa kocha wa makipa, akihudumu katika klabu za Yanga, Ihefu, Singida Blackstars, Fountain Gate, Namungo na timu mbalimbali za Taifa. Pia aliwahi kuwa msanii na kutoa nyimbo kadhaa za Bongo Fleva.

