BREAKING NEWS:BASI LAGONGANA USO KWA USO NA LORI. SHINYANGA

 

Ajali imetokea asubuhi ya leo Januari 27, 2026 majira ya saa 12:00 asubuhi, katika eneo la Mnadani, Kata ya Tinde, Halmashauri ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Ajali hiyo imehusisha basi la abiria la kampuni ya KISILE lenye namba za usajili T 229 EEL, lililokuwa likitoka Kahama kuelekea Mwanza, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo lililokuwa limebeba shehena ya mchele kutoka Dar es salaam kwenda Rwanda. 

Taarifa za awali zinaeleza kuwa juhudi za uokoaji zinaendelea huku vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo. Tutaendelea kuwajulisha taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana. Endelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii





Post a Comment (0)
Previous Post Next Post