Mkuu wa Wilaya(DC) ya Kibiti mkoani Pwani, Joseph Kolombo amewataka wakazi wa Wilaya ya Kibiti kufanya kweli kwa kujenga vyoo bora pamoja na sehemu ya kunawia mikono na maji tiririka.
Kolombo amesema hayo jana ofisi kwake wakati wa mahojiano malumu.
‘’Ujenzi wa vyoo bora ni ajenda yangu namba moja nimeshawaelekeza wakazi wa Kibiti kufanya kweli kwa kujenga vyoo bora. Ujenzi wa vyoo bora ni lazima iendane na sehemu nzuri ya kunawia mikono’’ amesema.
Katika hatua nyingine, Kolombo ameahidi kuendeleza kuhimiza wakazi wa Kibiti kutobaki nyuma katika suala zima la kufanya mazoezi.
‘’ Licha ya wananchi wengi kutopenda mazoezi, tutaendelea kuwahimiza kufanya kweli katika ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara hii itasaidia sana kuepuka magonjwa yasioambukizwa pamoja na mwili bwete’’ amesema.
Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Kibiti, Ammy Ally amesema kata yao inafanya kweli kwa kuondokana na matumizi ya kuni pamoja na vifuu. Amesema wakazi wengi kwa sasa hawajabaki nyuma katika kutumia nishati safi ya kupikia.
‘’Katika kipindi cha nyuma, wakazi wengi wa Kibiti walikuwa wanatumia kuni, vifuu ili kwa sasa wengi wameamua kufanya kweli kwa kutumia nishati safi ya kupikia’’ amesema.
Na Mwandishi - Kibiti

