Kamati ya hamasa imeendelea kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba siku ya 'Pamba Day' tarehe 10 Agosti 2024.
Kamati hiyo imeendelea kujigawa katika maeneo mbalimbali mkoani Mwanza kushiriki shughuli mbalimbali kuelekea Pamba Day ikiwemo kufungua matawi ya timu ya Pamba Jiji FC, kuuza tiketi na jezi ambapo leo Jumapili Julai 28,2024 hamasa imefanyika wilayani Magu.
Tiketi bado zimepatikana kwenye vituo vilivyotajwa, nunua tiketi yako mapema uwe sehemu ya historia
