WASANII 8 WA BENDI YA CRANE PERFORMERS WAKAMATWA KWA KUMTUSI RAIS MUSEVEN

 

Wasanii 8 wa Uganda wametiwa hatiani kwa kumdhihaki Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni.

Wasanii hao kutoka bendi ya Crane Performers wanaidaiwa kusema kuwa ‘walichoshwa kwa kusikiliza’ risala ndefu kutoka kwa Rais Museveni wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya ndoa kati ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi na Jacqueline Mbabazi, wikiendi iliyopita.

‘Tumechoka, achia kipaza sauti’, walisikika wasanii hao.



Vyombo vya habari vya nchini humo vinadai wanamuziki hao wa bendi ya Crane Performers walikuwa wakizungumza kwa lugha ya kienyeji ya Runyankole,

Walisema "Rutabandana Waturusya Rugahamuzindaro", ikimaanisha "spika, tumechoka, acha kipaza sauti"
Wanamuziki hao wanaripotiwa kuzuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kampala.
Wameshtakiwa kwa kumtusi rais, kulingana na faili za mahakama zilizoonekana na vyombo vya habari vya ndani.

By Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post