Katika orodha ya matajiri duniani iliyotolewa na Bloomberg inaonesha Mkurugenzi wa Meta Mark Zuckerberg amempiku kwa mara ya kwanza Mkurugenzi wa Tesla Elon Musk.
Zuckerberg amekuwa mtu wa tatu tajiri zaidi kwenye orodha hiyo ya Mabilionea ya Bloomberg siku ya Ijumaa, akiwa na utajiri wa dola bilioni 187 huku Elon Musk, akianguka hadi nafasi ya nne akiwa na utajiri wa dola bilioni 181.
Hii ni mara ya kwanza kwa Zuckerberg kuingia kwenye orodha ya tatu bora tangu 2020.
Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos yupo nafasi ya pili akiwa na utajiri wa dola bilioni 207 na Mkurugenzi Mtendaji wa LVMH Bernard Arnault yupo knafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa $223 bilioni.