Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mwalimu Hassan Masala
Mashindano ya DC CUP yamemalizika siku ya Jumamosi ya tarehe 24.02.2024,Ni mashindano yaliyo andaliwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mwl.Hassan Masala yakihusisha timu za mpira wa miguu ndani ya wilaya ya Ilemela kutoka katika kata mbalimbali,Fainali za mashindano haya yalikutanisha timu ya Capco Under 20 na Bawela fc, Dakika 90 zilimalizika hakuna timu iliyofanikiwa kufunga goli Ikalazimu waende kwenye mikwaju ya Penati na kuwafanya Bawela fc kuibuka washindi wa mashindano ya DC CUP 2024
Mshindi wa Kwanza apewa zawadi ya Jezi,Mipira,Medali,Ng'ombe nk..Na mshindi wa pili amepewa zawadi ya Jezi,mipira,medali na Mbuzi na Mshindi wa tatu amepata mpira na jezi pamoja na zawadi mbalimbali
Zaidi sana tumekuwekea Video hapo chini ya Matukio mbalimbali








