Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu kutoka Stanbic Benk Tanzania,Shangwe Kisanji Ametambulisha huduma iliyoboreshwa ya private banking.
Huduma ya private banking ni Mahususi kwa ajili ya wateja binafsi wenye ukwasi mkubwa. Huduma hii inalenga wafanyabiashara, wamiliki wa biashara, wawekezaji, wakurugenzi na wakuu wa vitengo mbalimbali katika mashirika na makumpuni binafsi.
Huduma hii kwa wateja wa Stanbic benk Ina manufaa makubwa sana ikiwemo kupata meneja mahusiano kwa ajili yake yeye familia yake ni huduma ambayo inaangalia katika kuhakikisha urithi wa Mali za familia zinafika vizazi vijavywo.
Ni huduma ambayo inaendakusaidia watoto wa wateja wetu kupata Elimu ya fedha anakuwa kuanzia miaka minane(8) mpaka anakwenda chuo.Huduma ambayo imejikita katika kutoa ushauri wa biashara, fedha, uwekezaji pamoja kufanya umahiri katika kuhakikisha Mali ya familia inafika vizazi vitatu hadi vitano huko chini.
Huduma hii inapatikana katika Jiji la Mwanza ,Dar es salaam, Arusha, Mbeya, Dodoma na hivi karibuni Geita na kahama.
Pamoja na hayo Amesema "Tumegundua na tumepata mrejesho kutoka kwa wateja wetu kwamba mtoto wangu hajui chochote kuhusu huduma ya fedha tumetembelea kwenye vyuo tumeona watoto wanapewa Boom alafu analitumia vibaya,Lakini huduma hii kwa ajili ya watoto ni mahususi kwa ajili ya kumsaidia mtoto aelewe hii shilingi mia tano ambayo mzazi ananipa siyo ya kwenda kununua pipi
Bali niwekeze sio kuhusu Ile shilingi mia Tano Bali ni tabia ambayo tunajaribu kuitengeneza atakapoanza kwenda chuo awe na uelevu katika matumizi yake ya pesa atakapokuja kuajiriwa aweze kujua faida ndogondogo kwa ajili ya kuongeza ukwasi wake faida za kutunza faida za kuwekeza lakini vilevile na faida za kutoa.
Pesa tuliyokuwanayo si kwa ajili tu ya matumizi Bali kwa ajili ya kuwekeza kutoa na kutumia kile kinachobaki.
Pamoja na hayo Pia Imetoa zawadi kwa Baadhi ya Wateja wao walioudhulia Uzinduzi huo
Na Maria Makenza