SAFARI YA MWISHO YA DKT ALOYSE KESSY AZIKWA MWANZA, VIONGO WASIFU UTENDAJI KAZI WAKE.

 

Aliyekuwa mganga mkuu wa Zahanati ya Polisi Mabatini mkoa wa Mwanza Mrakibu Mwandamizi wa (SSP) Ex. DKt  Aloyse Kessy ambaye alifariki dunia Januari 28,2025 amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Nyang'homango, Wilaya Misungwi huku viongozi mbalimbali wakisifu utendaji kazi wake.


Sifa hizo zimetolewa leo Februari 01.2025 na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, dini na wafanyakazi wenzake wakati wa ibada ya misa takatifu ya kumuombea marehemu Kessy iliyoongozwa na baba Paroko wa parokia ya Bukumbi, wilaya ya Misungwi Robert Ibengwe.


Sambamba na ibada takatifu ya kumuombea marehemu, viongozi na watu mbalimbali kupitia salam zao za pole, wamesifu maisha ya marehemu Kessy namna alivyokuwa anafanya kazi zake na kuishi mbele ya jamii na kutaka wafanyakazi wenzake na jamii kuiga maisha yake.


"Nichukuwe nafasi hii kuwaomba wananchi wa mkoa wa mwanza kuwa wavumilivu kwa janga hili lililotokea, kimsingi tumeshalipokea mwenzetu tulipanganae kusherehekea siku ya polisi day leo tarehe 01.02.2025 na alikuwa mstari wa mbele kuandaa na kumbe mungu alipanga polisi day kusherehekea yeye akiwa amelala hapa " amesema kamanda Mutafugwa


Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa geita Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo amewahasa wananchi na askari kuyaenzi mambo mema aliyoyaishi dkt kessy enzi za uhai wake .


"Jeshi la polisi  limepoteza mtu muhimu sana ambaye alikuwa na mipango mingi sana ya kuhakikisha hospital zote za Jeshi la polisi kanda ya ziwa zinasimama imara wananchi na askari wa Jeshi la polisi wanapata huduma bora " amesema SACP Jongo


Naye, Padri Fabian Mkoja amemuelezea marehemu dkt kessy namna alivyoishi na watu vizuri na amewaasa watu wote kuishi kwa kufata matendo mema aliyoyaishi. 



"Niwaase jamii katika nafasi mbalimbali tulizonazo tukumbuke kuwahudumia jamii kama Dkt kessy alivyofanya kwa upendo mkubwa na kwa unyenyekevu atakama alikuwa na madaraka makubwa lakini alijari upendo " amesema Fabian 




Na Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post