RC MTANDA AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA SSP DKT KESSY

 

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda leo Januari 31,2025 katika viwanja vya laini Polisi Mabatini ameongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kuaga mwili wa aliyekuwa mganga mkuu wa Zahanati ya Polisi Mabatini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Dkt Aloyce Kessy aliyefariki Januari 28,2025.


Akizungumza na waombolezaji, RC Mtanda amewahasa askari polisi na waombolezaji kumuenzi Dr Kessy kwa kufanya mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake katika kuihudumia Jamii.



“Naendelea kuwapa pole Jeshi la polisi kwa msiba huu, sisi tunaamini kila nafsi itaonja umauti Mungu amempangia kila mtu tarehe yake mwenzetu ameumaliza mwendo wake bila shaka ameumaliza vizuri kwa mujibu wa amelezo ya RPC Mutafungwa Dkt Kessy alikuwa na mwenendo mzuri mwenye bidi na jitihada hivyo tumenzi kwa hayo mazuri aliyotuachia”

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa amesema kifo cha Dkt Kessy kimewaumiza sana kutokana na kufariki ghafla na wakati bado Jeshi linamuhitaji kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi.

“Sisi Jeshi la polisi tunaiomba familia iwe na Subira katika kipindi hiki kigumu wamntangulize Mwenyezi Mungu kwa kila jambo hata sisi tumeumia sana kumpoteza mtu ambae alikuwa anajituma kwenye kazi zake, alikuwa na nidhamu ya hali ya juu, alikuwa na upendo kwa kila mtu”

“Wakati nampa taarifa   Afande IGP tarehe 28 pamoja na maafisa wenzake juu ya kifo cha Ofisa huyu akasema niwaombe familia muwe na Subira katika kipindi hiki kigumu na akanitaka nihakikishe anapumzishwa kwa amani kwenye nyumba yake ya milele kwa kuzingatia taratibu zote za kijeshi, kwakweli tumesikitika na kuumia sana kwa kifo cha Dkt Kessy”

Wakati wa misa ya kumuombea marehemu iliyoongozwa na Padre Pamphilius Madata wa Parokia ya Kiloleli amewaasa askari polisi kutekeleza wajibu wao kadri inavyotakiwa kwa kusimamia sheria kama alivyokuwa anafanya marehemu Dkt Kessy


tujisikie vizuri kwenye kutekeleza wajibu wetu tusichoke kufanya yaliyo mazuri, tusichoke kumuabudu mwenyezi Mungu licha ya vyeo tulivyonavyo, tuwe madaraja ya kuunganisha watu na kutekeleza wajibu wetu ipasavyo Dkt Kessy amefariki akiwa anayatenda yaliyo mema kwahiyo tuyaishi hayo aliyotuachia” amesema Madata.

Kwa upende wake kaka wa marehemu Leonard Kessy kwa niamaba ya familia ametoa shukrani kwa Jeshi la Polisi kwa ushirikiano walioutoa tangu umauti umemkuta ndugu yao hadi leo wakati wa kutoa heshi zao za mwisho.

Dkt Kessy anatalajiwa kuzikwa kesho Februari 1,2025 katika eneo la Bukumbi wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.






Na Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post