Lavrov na Rubio kukutana Riyadh kuijadili Ukraine

 

Viongozi waandamizi wa Urusi na Marekani wanatarajiwa kukutana nchini Saudi Arabia kwa mazungumzo ya awali ya kumaliza vita vya Ukraine na kurekebisha mahusiano yaliyopwaya kati ya Moscow na Washington.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov  atakuwa na mazunngumzo na mwenzake wa Marekani Marco Rubio pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa pande hizo mbili mjini Riyadh kesho Jumanne. 

Mazungumzo hayo yanafanyika baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwasiliana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita na kuwaamuru maafisa wao kuanza majadiliano ya kumaliza vita vinavyoendelea. 

Hata hivyo Ukraine haitowakilishwa kwenye mazungumzo hayo ya Riyadh, na kiongozi wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskiy amesema hawatayakubali matokeo ya mkutano wowote utakaojadili kumaliza vita bila ya Ukraine kuhusishwa
 

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post