BASATA Yapongeza Waandaaji wa Tuzo za Ucheshi, Yasema Lengo ni Kukuza Sanaa

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana, amepongeza waandaaji wa Tuzo za Ucheshi kwa mchango wao katika kuinua sekta ya sanaa nchini.

Akizungumza leo katika All-Star Comedy Festival lililofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dkt. Mapana alisisitiza kuwa BASATA lipo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa, si kwa ajili ya kufungia wasanii.


“Tunataka kuona sanaa inakua na wasanii wakinufaika na kazi zao. Ndiyo maana tunashirikiana na wadau wote kuhakikisha tasnia inazidi kustawi,” alisema Dkt. Mapana.

Tukio hili limewakutanisha wadau mbalimbali wa sanaa na burudani, huku likiwa sehemu ya maandalizi ya Tuzo za Ucheshi zinazotarajiwa kufanyika tarehe 22 Februari 2025.



Na Mwandishi  Wetu-Dar es salaam

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post