Lengo la misako na doria hizo ni kuzuia, kukamata na kuwafikisha mahakamani
watuhumiwa wa makosa mbalimbali tuliokuwa tunawasaka baada ya kupata taarifa zao
za uhalifu kupitia mikutano ya hadhara ya ushirikishwaji jamii ambayo tumekuwa
tukiifanya katika maeneo mbalimbali ikiwemo visiwa vya Ikulu, Chemagati, Chembaya,
Zilagula, Mchangani, Ntama, Soswa, Nyamango, Yozu, Nyanzune, Bihira, Ito na
mialo ya Kijiweni, Itabagumba, Kaunda na Kanyala. Mikutano ya ushirikishwaji wa jamii
ililenga kuwapa wananchi elimu ya uvuvi salama, mazingira salama, ulinzi jirani na
uundaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi kupitia viongozi wa vitongoji, vijiji na kata.
Aidha, tumekamata vielelezo mbalimbali ikiwemo mitumbwi 6 isiyokuwa na namba za
usajili ambayo inatumika kufanya wizi wa mazao ya uvuvi, mashine moja ya kuendeshea
Boti, nyavu haramu vipande 1,500 aina ya timba (Mono filaments), Bhangi kilogramu 5
na pombe haramu ya moshi lita 30. Sambamba na hayo Jeshi la polisi linaendelea na
hatua mbalimbali za kiuchunguzi dhidi ya uhalifu na wahalifu na mara zitakapokamilika,
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote ikiwemo kuwafikisha
mahakamani.
Miongoni mwa watuhumiwa hao 115, watuhumiwa 31 wamefikishwa mahakamani
ambapo watuhumiwa 11 wamehukumiwa kwenda jela miezi 12 baada ya kupatikana na
hatia ya kujihusisha na ukahaba na watuhumiwa 20 kesi zao zinaendelea na zipo katika
hatua mbalimbali, watuhumiwa wengine 81 watafikishwa mahakamani mara baada ya
upelelezi kukamilika
Operesheni hii ni endelevu na tutahakikisha tunafika visiwa vyote vya mkoa wa Mwanza,
hivyo Jeshi la polisi mkoa Mwanza linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono
jitihada za kiusalama zinazofanywa na Jeshi la polisi ili kudumisha amani na usalama.
Pia, tunawaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yao.
.jpeg)


