POLISI MWANZA:YAWATOA HOFU WANANCHI UWEPO WA MTU MMOJA MBAKAJI,KULAWITI NA KUJERUHI JINA ‘TELEZA’

 

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linapenda kuwatoa hofu wananchi wa mkoa wa Mwanza hususani wakazi wa kata ya Mkolani na Buhongwa juu ya uvumi wa taarifa potofu zilizoenezwa kwenye maeneo hayo zikieleza juu ya mtu aitwaye Teleza na anayedaiwa kubaka, kuwalawiti wanawake na kuwajeruhi.


 Aidha, Jeshi la polisi linalaani kitendo cha baadhi ya wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kutaka kumshambulia mwananchi eneo la mtaa wa Ibanda, katika nyumba ya kulala wageni, kata ya mkolani, wilaya ya Nyamagana, majira ya 10:00hrs ambaye tulifanikiwa kuokoa maisha yake ambapo walimtuhumu kuwa ni Teleza na wakidai kwamba ndiye anaye wabaka na kulawiti wanawake wa maeneo hayo. Taarifa hizo sio za kweli bali ni zakufikirika na kutokana na kitendo hicho, 





Jeshi la polisi hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wataobainika kuhusika kutenda uhalifu huo ikiw

emo wanaochapisha na kutoa taarifa potofu kwa wananchi kwani zinaweza kuleta taharuki na uvunjifu wa amani. Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa yoyote ya uhalifu au viashiria vya uvunjifu wa amani watoe taarifa kwa Jeshi la polisi ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.





Na Pascal Kadushi


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post