Mpaka wa Kongo-Rwanda wafungwa baada ya M23 kuiteka Goma

 

Mpaka kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) karibu na mji wa Goma uliojaa majeshiumefungwa Jumatatu, chanzo kutoka ubalozi wa Ulaya na mashahidi walisema, saa chache baada ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Rwanda kuingia mji huo mkuu wa mkoa wa Kongo Mashariki. Rwanda imekana kuhusika licha ya ripoti za kuaminika kutoka Umoja wa Mataifa kuonyesha kuwa inawaunga mkono waasi wa M23.

"Mpaka umefungwa," kilisema chanzo cha ubalozi katika mazungumzo na shirika la habari la AFP. "Hakuna anayekuja, hakuna anayekondoka, isipokuwa baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na familia zao waliohamishwa asubuhi hii," alisema mfanyakazi wa misaada katika kivuko kikuu cha mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Waasi pia wameufunga uwanja wa ndege wa Goma na kuchukua udhibiti wa kituo cha redio cha serikali kilichokuwa kikiendelea kucheza muziki. Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa, Bintou Keita, alikiambia kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumapili usiku kwamba "tumekwama," huku uwanja wa ndege ukiwa umefungwa na barabara zote zimefungwa.

Jumatatu asubuhi, kulikuwa na ripoti kuwa maelfu ya wafungwa walitoroka baada ya jela kuu ya Goma kuvunjwa. Uporaji na milipuko ya silaha ilisikiwa huku wakazi wakikimbia au kujificha ndani.

Soma pia: Waasi wa M23 waingia Goma

Baadhi ya wanajeshi wa Kongo walijisalimisha kwa vikosi vya ulinzi vya Umoja wa Mataifa baada ya muda wa mwisho wa waasi wa M23, huku wengine wakikimbia kwa mashua kuvuka Ziwa Kivu kuelekea Bukavu. Wengi wa wapiganaji wa kigeni kutoka Romania na Bulgaria waliokuwa wakipigana upande wa jeshi la Kongo walifanikiwa kuondoka Goma katika dakika za mwisho. Baadhi yao wamekabidhi silaha zao kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Waasi wa M23 sasa wanafanya upekuzi katika nyumba na hoteli ili kuangalia kama kuna wanajeshi waliojificha huko.

"Ninaogopa mauaji ya kimbari yanaweza kutokea watakapofika. Mahali ambapo M23 tayari imechukua vijiji, wamewaua vijana," Paul Buyana aliiambia DW siku moja kabla ya kundi hilo la waasi kuchukua udhibiti wa Goma.

Kilichoongeza wasiwasi kwa mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 27 kutoka Kongo ni kushindwa kwake kupata kazi, kwani wamiliki wa biashara wanahofu ya wapiganaji au waporaji waliokuwa wakifyatua risasi mjini.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post