Makubaliano hayo, yaliyotangazwa Jumatano jioni na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, yanajumuisha kuwachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina walioko katika magereza ya Israel.
Usitishaji huu wa vita unatarajiwa kuanza Jumapili na utaendelea kwa siku 42, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa pande hizo kusitisha mapigano tangu vita vilipoanza tena Gaza miezi 15 iliyopita.
"Makubaliano haya yanatoa matumaini kwa raia wa pande zote ambao wamepitia mateso makubwa,” alisema Al Thani, akihimiza pande zote kudumisha utulivu wakati wa utekelezaji wa makubaliano hayo.
Katika awamu ya kwanza, Hamas itawaachilia huru mateka 33 wa Kiyahudi, wakiwemo wanawake, raia, watoto, wazee, na askari wanawake. Kwa upande mwingine, Israel itawaachilia huru wafungwa kadhaa wa Kipalestina.Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al ThaniSheikh Al Thani, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika mazungumzo haya, alielezea matumaini yake kuwa usitishaji vita huu utatoa msukumo kwa mazungumzo ya amani ya baadaye.
Rais wa Israel ametoa wito kwa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuidhinisha rasmi makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza.


