Wakazi wa Mtaa wa busenga kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela,Wanakwenda kuondokana na tatizo la uhaba wa Umeme wakutosha katika Mtaa wao wenye zaidi ya Kaya 1800 na Wananchi wapatao zaidi ya 3000.Eneo lao limekua na changamoto ya muda mrefu la kua na Umeme mdogo jambo ambalo linawafanya washindwe kupiga hatua ya kimaendeleo kutokana na changamoto hiyo
Kwa Upande wake Meneja TANESCO Mkoa
wa Mwanza Eng. Godlove Mathayo amesema eneo la busenga ambalo lilikuwa na
changamoto ya ukosefu wa umeme kwa muda
mrefu Sasa limepata ufumbuzi kwa sababu bajeti imetoka na jambo hilo
litatekelezwa hivi karibuni.
Ameyasema hayo mapema hii Leo huku akisema kuwa bajeti
iliyotolewa ni sh milioni 40 ambayo itatosha kurekebisha matengenezo yote.
Aidha amewashukuru wananchi wote kwa kujitoa na kuwa wavumilivu kwa kipindi chote Cha changamoto hiyo ya umeme,na ndani ya mwezi Novemba mwaka huu kazi itakua imekwisha
Kwa Upande wake Diwani wa kata ya buswelu Sarah Paul Ng'wani amemshukukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluh Hassan kwa kutenga fedha hizo ambazo ni sh milioni 40 kwa ajili ya matengenezo na kuwaona wakazi ya busenga kata ya Buswelu na kuwafikia kwa ajili ya kuwatatulia tatizo hilo lililodumu kwa muda mrefu.
Aidha amemshukuru meneja wa TANESCO kwa kufikia na kuwatatulia changamoto
hiyo ya ukosefu wa umeme iliyowasumbua kwa muda mrefu.
Pia amewaomba wananchi wote kutunza miundombinu ya umeme na
kuilinda na pia kuwa waangalifu Ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa mtaa wa Busenga aliyemaliza muda wake,Shokha Mhango amewashukuru
TANESCO kwa kujitoa na kuwafikia Ili kuwatatulia changamoto ya ukosefu wa umeme
ambayo imewasumbua kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo na kuwaasa wananchi wote kufanya kazi kwa
bidii kwani walikuwa hawafanyi kazi kwa sababu ya ukosefu wa umeme.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh Samia Suluh Hassan kwa kuwakumbuka na kusikia maombi Yao.
Sambamba na hayo wananchi wameiomba serikali kuwasaidia kuwafungia umeme katika shule ya msingi Busenga kwani itasaidia watoto kujifunza zaidi kwa vitendo.
Wameahidi kuitunza miundombinu Ili iweze kudumu kwa muda
mrefu kwa ajili ya matumizi Yao ya kujipatia kipato.
NA MARIA MAKANZA















