POLISI GEITA INAMSHIKILIA FUNDI SEREMALA KWA MAUAJI

 

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia Athumani Issa Baseka, Miaka 39, Fundi Seremala, Mkazi wa Kamhanga Wilayani Geita kwa tuhuma za Mauaji ya Faida Deus Lucas, Miaka 34, Msukuma, Mkulima wa Bugalama.

Ni kwamba mnamo tarehe 30.10. 2024 majira ya saa sita usiku huko Kitongoji cha Mwamashiki Kijiji na Kata ya Bugalama Wilaya ya Geita ambapo mtuhumiwa alimuua Faida Deus Lucas, kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani utosini, kisogoni na shavu la kushoto baada ya kumkuta marehemu akiwa na mke wa mtuhumiwa ambaye jina tunalihifadhi kwa sababu za kiupelelezi.


Mtuhumiwa Athumani Issa Baseka na mke wake walikuwa na mgogoro wa kifamilia; ndipo mwanamke huyo akaondoka na kwenda nyumbani kwao. Alipofika huko alianzisha mahusiano ya kimapenzi na marehemu Faida Deus Lucas. Upelelezi unakamilishwa mara moja na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria na uchunguzi kukamilishwa.

Jeshi la Polisi linawaasa wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi. Watakaobainika watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.

NA MWANDISHI WETU | GEITA
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post