MENDING KIDS INTERNATIONAL YAINGIA MAKUBALIANO NA MUHIMBILI YA KUBORESHA HUDUMA NA KUTOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA TZS. 250 MIL

 

Shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la nchini Marekani linalojihusisha na kusadidia matibabu kwa watoto, kutoa msaada wa vifaa tiba pamoja na wataalam (MENDING KIDS INTERNATIONAL) leo limeingia makubaliano na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na kutoa msaada wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kufanyia upasuaji kwa watoto wenye changamoto za shingo na njia ya hewa wenye thamani ya TZS. 250 Mil.

Akizungumza mara baada ya kuingia makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema makubaliano hayo yanalenga kuwaongezea ujuzi wataalam wa hospitali hiyo pamoja na kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba ambavyo havipo nchini kwani kupitia makubaliano hayo watoto wenye changamoto hizo wataweza kupata huduma hizo bila kuzifuata nchi za nje.






“Tumekusanya watoto takribani 22 ambapo tutawafanyia upasuaji ambao wamekua na changamoto hizo kwa muda mrefu lakini pia kupitia makubaliano haya yatasidia kuleta wataalam kila baada ya miezi mitatu ambapo sisi hospitali malengo yetu ni wataalam hao waje kwa mwaka mara nne hivyo tutaweza kutoa huduma bora za kibingwa na ubingwa bobezi,” amefafanua Prof. Janabi.

Kwa upande wake rais wa bodi wa shirika hilo Dkt. Ayal Wilner ameupongeza uongozi wa MNH katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora za kibingwa na ubingwa bobezi ambapo ameahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha kufikia malengo yaliyokusudiwa na pia kubailishana uzoefu wa kujifunza zaidi kwa kufanya kazi pamoja na wataalam wa hospitali hiyo.

Na Mwandishi wetu -Dar

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post