LORI LAUA WANACHUO WAWILI.KILIMANJARO

 

Wanafunzi wawili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyapori kilichopo Moshi Mkoani kilimanjaro wamefariki Dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo November 03,2024 eneo la Tuli Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema waliofariki ni Evanc David Lyimo na Ebenezer Benkars Isangya wote Wenyeji wa Moshi na ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa Dereva aliyekuwa anaendesha bila kufuata kanuni za usalama barabarani

“Kuna tukio la ajali ya gari kuacha njia na kupinduka na kusababisha vifo na majeruhi usiku wa kuamkia leo ambapo gari lenye namba za usajili SU.41476 Kamazi lori lililokuwa linawapeleka Wanachuo hao 40 Wilayani Mlele Mkoani Katavi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo liliacha barabara na kupinduka na kusababisha kifo cha Mtu mmoja papohapo”

“Baadaye majeruhi mmoja akafariki hivyo kufanya vifo kuwa viwili pamoja na majeruhi saba wote Wanaume lakini pia majeruhi wengine wanaendelea na matibabu chanzo cha ajali hii ni uzembe wa Dereva uliopelekea kushindwa kulimudu gari na kusababisha ajali hiyo”

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post