ELIMU YATOLEWA KWA WAVUVI.MWANZA

 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeanza Operesheni maalum ya kuwasaka wezi wa nyavu za uvuvi katika ziwa victoria sambamba na kutoa elimu.


Hayo yamejiri leo Novemba 12,2024 katika mwalo wa Luchelele wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati Mkuu wa kikosi cha Polisi wanamaji mkoa wa Mwanza Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Wenceslaus Muchunguzi alipokutana na wavuvi na wananchi wa eneo hilo na kuwapa elimu ya uvuvi salama.



Sambamba na elimu hiyo Muchunguzi amewataka wananchi wa eneo hilo kuacha vitendo vya wizi wa nyavu za uvuvi za watu wengine na kuacha kutumia zana haramu za uvuvi.


"Eneo hili la Luchelele limeonekana ni eneo ambalo watu wengi wanaokuja hapa si kwa jili ya kuvua ni kwa ajili ya kuiba zana za wenzao" amesema Muchunguzi 


Aidha, ASP Muchunguzi amewahakikishia wananchi wa eneo hilo kwamba Jeshi la Polisi litaendelea na doria kwa kushirikiana na taasisi nyingine ili kukagua vifaa vya kujiokolea vinavyotakiwa kuwepo katika kila mtubwi ikiwemo maboya ili kila abiria aweze kujiokoa pale inapotokea dharula wawapo safarini katika ziwa victoria.


Naye, Elikana Masigili mvuvi katika mwalo wa Luchelele amewaasa wamikiki wa mitumbwi kuweka alama za kudumu kwenye nyavu zao ikiwemo kupaka rangi moja kwenye nyavu zao zitakazo wasaidia kutambua kwa haraka kuliko kila nyavu kuwa na rangi tofauti jambo linalochangia kuendelea kwa vitendo vya wizi wa nyavu.


Na Pascal Kadushi
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post