YAJUE MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA KEMIKALI YA ZEBAKI (MEKYURI) KWA WACHIMBAJI WA MADINI

 

Dkt. Befrina Igulu ambaye ni mratibu wa mradi wa udhibiti wa matumizi ya Zebaki (Mekyuli) kwa wachimbaji wadogo amesema Baraza la Taifa na uhifadhi wa mazingira limetoa  mamlaka na dhamana  kwa Baraza la Taifa la uhifadhi wa mazingira  kusimamia hifadhi ya mazingira kwa lengo la kulinda afya ya jamii.


Ameyasema hayo mapema hii Leo huku akisisitiza kuwa hii imetolewa mahususi kwa ajili ya kulinda afya ya jamii pamoja  na mifumo ya ikolojia na kuhakikisha maendeleo endelevu ya jamii kwa watanzania.



Aidha ameongeza kuwa Baraza Linajuhudi nyingi mojawapo ikiwa ni kusimamia tathmini athari za mazingira lakini ufatiliaji na uzingatiaji wa Sheria za mazingira lakini pia kufanya tafiti za kimazingira ambazo zinasaidia serikali kwenye kufanya maamuzi sahihi ambayo yanalinda afya ya jamii na mazingira ya eneo husika.


Pia tafiti inasaidia kuleta miradi mbalimbali ambayo inasaidia kuratibu na kuhakikisha kurudisha afya ya mazingira katika Hali ya kawaida.
Katika sekta ya uchimbaji mdogo Zebaki au Mekiul  imezoekeka kama kemikali ambayo imekuwa ndio kiungo muhimu cha kukamatisha dhahabu.

Lengo la mkataba huu ni kupunguza matumizi ya Zebaki katika uchanjuaji wa dhahabu na uchimbaji mdogo ni kati ya sekta kubwa sana nchini na pia ni kitega uchumi Cha watu wengi hasa kwa ukanda huu wa ziwa.

Madhara ya Zebaki katika afya inaathiri mfumo wa Neva ambayo ndio mifumo ya fahamu pia inapekekea msongo wa mawazo, kupungua fahamu, kuathirika kwa Figo  kwa sababu hua inaenda kushambulia viungo laini kama moyo Figo, ubongo pamoja na kupoteza usikivu na uonevu na kutetemeka kwa wachimbaji wanaokaa muda mrefu machimboni.
Sifa ya Zebaki  ipo katika hali ya kimiminika na inasafiri masafa merefu na haibadiliki  na inaweza ikasafiri katika hiyo Hali kutoka katika mfumo mmoja kwenda katika mfumo mwingine.
Chanzo 

Kwa Upande wake Meneja wa Mawasiliano NEMC Irene John ameeleza madhara yatokanayo na Zebaki na kuwaomba wanahabari kutoa Elimu kwa Jami.



Ameyasema hayo hii Leo akiwa na wanahabari na kuwaasa kurusha habari hizi za madhara ya Zebaki kwani  zina madhara makubwa kwa jamii.

Aidha amemalizia kwa kusema kuwa Vyombo vya habari vya mikoani ndivyo vinavyosikilizwa sana hvyo wanapaswa kurusha habari hizi katika vipindi mbalimbali.






















Na Maria Makanza.





Post a Comment (0)
Previous Post Next Post