AFISA Lishe wa mkoa wa Pwani David Vuo amesema mkoa wa Pwani utaendelea kuhamasisha wakazi wa mkoa huo kutobakia nyuma katika kuzingatia Lishe bora. Vuo alitoa Rai hiyo jana wakati wa mahojiano malumu.
‘’Pwani katika Lishe tunaongoza mwaka 2023 tulichukua tuzo ya kuwa mkoa wenye kiwango cha juu sana kwa wananchi wake kuzingatia suala la lishe bora.’’ amesema Vuo.
Akielezea zaidi kuhusu lishe bora, Vuo amesema kauli mbiu ya Fanya Kweli, usibaki nyuma imewasaidia wakazi wa Pwani kuongeza hari na kuacha kufanya mambo kwa mazoea.
‘’Tunashukuru sana viongozi wetu wa Pwani,wanaendelea kufanya kweli kwa kutuongoza vizuri na kuhakikisha lishe bora katika jamii inakuwa kipaumbele’’ amesema.
Naye katibu Tawala wa mkoa wa Pwani(RAS) Rashid Mchatta amesema kuhusu lishe wanafanya kweli kwa kushirikiana na wazazi pamoja na wadau ili kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni.
Na Mwandishi wetu,Pwani

