WIZARA YA MADINI YAVUNJA REKODI UKUSANYAJI WA MADUHULI

 

Ndani ya miezi miwili yakusanya shilingi bilioni196 ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2015/2016 cha shilingi bilioni 161

Waziri Mavunde apongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa kuibeba Sekta ya Madini kupitia ukusanyaji wa maduhuli.

Ampongeza Rais Samia kwa kuipa kipaumbele Sekta ya Madini kwa kuongeza bajeti kwa mwaka 2024/2025

Atoa maagizo matano kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa wa Tanga


Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amepongeza maafisa madini wakazi wa mikoa kwa kuvunja rekodi ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 196 kwa kipindi cha miezi miwili katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi ambacho ni zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 161 kilichokusanywa kwa mwaka mzima wa fedha 2015/2016.

Mhe. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Septemba 15, 2024 kupitia kikao chake na menejimenti ya Tume ya Madini ikiwa ni pamoja na wakurugenzi, mameneja na maafisa madini wakazi wa mikoa chenye lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha Sekta ya Madini katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 kupitia ukusanyaji wa maduhuli, udhibiti wa utoroshaji wa madini, udhibiti wa mianya ya upotevu wa makusanyo na kuimarisha usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.


Wengine waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya Samamba, Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Buriani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Jafari Kubecha.
Amesema kuwa tangu kufanyika kwa maboresho ya Sheria na kanuni za Madini, kupitia Tume ya Madini, Wizara ya Madini imeendelea kuongeza kasi ya ukusanyaji wa maduhuli kutoka mwaka hadi mwaka siri ikiwa ni ubunifu wa ukusanyaji wa maduhuli kwa kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri sana ya ukusanyaji wa maduhuli hasa katika kipindi za kuanzia mwezi Julai hadi sasa ambapo kiasi cha shilingi bilioni 196 zimekusanywa, kiasi ambacho kinazidi kiasi kilichokusanywa kwa mwaka mzima wa fedha wa mwaka 2015/2016,” amesisitiza Mhe. Mavunde.

Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde ametumia fursa hiyo kumponge


Na mwandishi wetu- Tanga

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post