WACOMORO KUTIBIWA TANZANIA

 

Wananchi wa Visiwa vya Comoro sasa watatibiwa Tanzania kwa huduma za Afya walizokuwa wakizafata Ulaya na Mashariki ya Mbali.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Moustadroine Abdou, akiongea na waandishi wa habari leo, amesema sasa wananchi wa Comoro hawana haja ya kusafiri mpaka Ulaya na Mashariki ya Mbali kufata huduma za Afya.

"Huduma tulizokuwa tunazifata Ulaya na Asia kama upandikizaji wa figo kumbe tunaweza kuzipata hapa Tanzania," amesema Mhe. Spika wa Bunge wa Muungano wa Visiwa vya Comoro alipotembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).


Mhe. Spika wa Visiwa vya Comoro ametembelea Idara za Magonjwa ya Moyo, Huduma ya Upandikizaji Uloto (Tiba ya Sikoseli), Idara ya Radiolojia (MRI), Kliniki maalumu ya Viongozi na Wodi ya Rais katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel, amesema ziara hiyo imempa fursa Mhe. Spika wa Bunge wa Visiwa vya Comoro kushuhudia mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya.


Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel, amesema ziara hiyo imempa fursa Mhe. Spika wa Bunge wa Visiwa vya Comoro kushuhudia mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya.

"Pia mradi wa Kituo cha Nuclear Medicine cha BMH umefikia Asilimia 50. Kituo hiki kitakuwa ni Kituo cha Umahiri wa Matibabu ya Saratani katika Afrika. Tutashirikiana na Chuo Kikuu cha Havard cha Marekani," amesema Naibu Waziri wa Afya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt. Kessy Shija, amesema BMH inahudumia zaidi ya wananchi milioni 14 katika Kanda ya Kati na mikoa ya jirani.

"BMH tunatoa huduma za Afya za ubingwa wa kati na ubingwa wa juu kama upandikizaji wa figo na upandikizaji uloto ambayo ni tiba ya sikoseli," amesema Dkt Shija kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Prof Abel Makubi.


Dkt. Shija ameongeza katika ushirikiano huu wa BMH na Visiwa vya Comoro, Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) itafanya huduma mkoba (medical outreach) katika Visiwa hivyo vilivyopo Kusini Mashariki ya Afrika.

"Ushirikiano pia utahusisha mafunzo kwa wataalamu kutoka Comoro kuja kufanya mafunzo ya vitendo hapa BMH," amesema Dkt Shija

Na Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post