Mhe. Mtanda akizungumza na wananchi hao waliojitokeza kwa wingi katika mazishi ya mwananchi mwenzao amesema, wakati anapita barabarani ameshangazwa kuona idadi ya watu wengi wakiwa wamekusanyika na kuamua kusimama kujionea nini kinaendelea.
Aidha RC Mtanda amesema amefurahishwa kuona mashabiki wa timu ya Simba na Yanga wakiwa wamekusanyika pamoja huku wakiwa na jezi zao katika msiba huo jambo ambalo limemshangaza sana.
"Nimefurahishwa sana na utamaduni mzuri wa mashabiki wa timu hizi zenye utani wa jadi kuja kumpa kampani mwenzenu wa timu ya yanga aliyepata msiba, Ninawapongenzi".
Lakini hii pia inaashiria kwamba kumbe michezo ni utani wa jadi ambao wakati wa furaha tunakua wote na wakati wa huzuni tunakuwa wote. Ameongeza Mhe. Mtanda.
Sambamba na hayo RC Mtanda amesema kwa kuwa ameona hapo Kijijini Ilenze kuna mashabiki wa michezo wengi, ameahidi kuleta wataalamu kutoka Mkoani kuja kufungua tawi la timu ya Pamba Jiji ambayo ndio timu ya Mkoa wa Mwanza.
Na Pascal Kadushi






