Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi limefanikiwa kuokoa watu 29 ambao walizama maji katika ziwa Victoria wakati mtumbwi waliopanda kutoka Mwalo wa kirumba kwenda katika kisiwa cha Goziba kilichopo wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera ulipogonga mwamba katika eneo la Bwiru wilaya ya Ilemela hatimaye mtumbwi huo kupinduka na kuzama ukiwa na watu na mizigo.
Mnamo tarehe 25.09.2024 majira ya 17:10 hrs katika mwalo wa Bwiru wilaya Ilemela mtumbwi wenye namba za usajili TMZ 012212 unaomilikiwa na Amoni John Lutabanzibwa ujulikanao kwa jina MV SEA FALCON ukiwa na abiria wanaokadiriwa kuwa 31, Nahodha na msaidizi wake, uliondoka katika mwalo wa Kirumba kuelekea katika kisiwa cha Goziba kilichopo wilaya ya Muleba mkoa Kagera. Mtumbwi huo pamoja na abiria pia ulibeba mizigo.
Taarifa kuhusiana na ajali hiyo ziliripotiwa polisi na hatua za uokozi kuanza mara moja ambapo boti ya polisi BP 29 CHATU iliyokuwa doria ilifika eneo la ajali na kushirikiana na wananchi (wavuvi) na kufanikiwa kuwaokoa abiria 29 waliokuwa ndani ya mtumbwi huo. Wahanga wa ajali hiyo walikutwa wakiwa wanaelea kwenye maji huku wakiwa wameshikilia madumu ya mafuta na wengine wakijitahidi kuogelea kwa ajili ya kujiokoa, walifikishwa nchi kavu na kupatiwa huduma ya kwanza kisha walipelekwa hospital ya mkoa Sekou-Ture kwa matibabu ambapo 14 walitibiwa na kuruhusiwa, 14 bado wanaendelea na matibabu kati yao 6 ni wanawake na 8 ni wanaume, kwa ujumla hali za afya zao zinaendelea vizuri.
Jitihada za uokozi ziliendelea zikishirikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wananchi na wadau wa sekta ya uvuvi ambapo tulifanikiwa kuokoa mali mbalimbali za abiria ambazo ni madumu 58 ya mafuta ya Petrol yenye ujazo wa lita 270, katoni 100 za maji pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani. Jitihada za kutafuta mtumbwi huo uliozama kwenye maji zinaendelea kwa kuwashirikisha wazamiaj
Katika ajali hiyo kwa mujibu wa maelezo ya Nahodha na msaidizi wake ulikuwa na abiria 31 ambapo watu 29 wameokolewa wakiwa hai, mmoja amepatikana akiwa amefariki dunia ambaye ametambuliwa kwa jina la Kharidi Rajabu, miaka 6, mwanafunzi wa darasala la kwanza katika shule ya msingi Goziba, wilaya ya Muleba na mtu mwingine ambaye hajulikani jina aliyekuwepo katika ajali hiyo bado tunamtafuta. Waliokolewa majina yao ni:-
1. Robert Kabota, miaka 31, nahodha wa mtumbwi, makao- kitangili.
2. Salum Shaban, miaka 59, msimamizi wa mtumbwi, makao - Kabuholo-Kirumba.
3. Lucia Kubagwa, miaka 47, mfanyabiashara, makao-nyarugusu, Geita.
4. Okinyi Rafael, miaka 47, mkulima makao- nyamburi rorya,
5. Jackson Magulu, miaka 29, mvuvi, makao- Buselesele Geita.
6. Elia Marco, miaka 29, mrundi, mkulima, makao - Burundi,
7. Siwema John, miaka 28, mfanyabiashara, makao- Kisesa Magu.
8. Ladislaus Kongoka, miaka 44, mkulima, makao-Nyehunge-Sengerema.
9. Salimu Hamis, miaka 20, mfanyabiashara, makao-Sengerema Mjini.
10.Karaudini Ishengoma, miaka 23, Baharia, makao - Kiloleli-Ilemela
11.Petro Joseph, miaka 39, mkulima, makao-Katoro Geita.
12.Richard Elize, miaka 18, mrundi, mkulima, makao- Burundi.
13.Said Issa, miaka 22, mkulima, makao- Kigarama-Kagera.
14.Noris Mwene, miaka 38, mfanyabiashara, makao mbagala-Dar Es Salaam.
15.Juma Elimerick, miaka 43, mvuvi, makao- Shibula-Ilemela.
16.Salum Totimu, miaka 36, mkulima, Makao-Ibanda Ilemela.
17.Samwel Odondo, miaka 53, mfanyabiashara, makao-Tabata-Segerea.
18.Ramadhan Abdul, miaka 29, mkulima, makao- Kashrazi-Ngara.
19.Isomba Myamwezwa, miaka 47, mfanyabiashara, makao- Igunga-Tabora.
20.Andre Willson, miaka 48, mjasiliamali, makao- nyanguge-Magu.
21.Idrisa Juma, miaka 22, mkulima, makao- gozba-muleba.
22.Mussa Japhet, miaka 31, mvuvi, makao- pasians-Ilemela.
23.Nemeima Silive,miaka 22, mrundi, mkulima, makao- Burundi.
24.Elias Michael, miaka 29, mkulima, makao- Ngara-Kagera.
25.Amon Safari, miaka 45, mkulima, makao- katoro-Geita.
26.Edward Mghana, miaka 25, mvuvi, makao- Goziba-Muleba.
27.Aisha Twalibu,miaka 29, mfanyabiashara, makao- Katoro-Geita.
28.Mariam Paschal, miaka 40, mkulima, makao- Igombe-Ilemela.
29.Rudia Malegesi, miaka 55, mkulima, makao- Kitangiri-Ilemela na
30.Salome Kefa, miaka 29, mkulima, makao nyanguge-Magu.
Chanzo cha ajali hiyo ni mtumbwi kugonga mwamba, kutoboka na kuingiza maji ndani ya mtumbwi. Kufuatia ajali hiyo, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watatu ambao ni:- Amon John Lutabanzibwa, miaka 46, mfanyabiashara na mkazi wa mtaa wa Buswelu ambaye ni mmiliki wa mtumbwi huo, Robert Kabota , miaka 31, nahodha wa mtumbwi, mkazi wa kitangili na Salum Shaban, miaka 59, msimamizi wa mtumbwi na mkazi wa mtaa wa Kabuholo-Kirumba ambao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo kwani mtumbwi huo haukuwa na kibali cha kubeba abiria kutoka shirika la Uwakala wa Meli Tanzania ( TASAC).
Aidha, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linazidi kuwakumbusha wananchi hususani wasafirishaji wa vyombo vya majini kuendelea kuzingatia sheria na taratibu za usalama wa vyombo vya majini ambazo zinawataka wamiliki wa mitumbwi kutoa huduma ya usafiri kwa kuzingatia masharti ya leseni zinazotolewa na mamlaka husika (TASAC). Pia, Jeshi la Polisi linawakumbusha wananchi kutoendelea kupanda mitumbwi iliyosajiliwa kubeba mizigo kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa maisha yao hivyo wanapaswa kupanda vyombo vilivyosajiliwa kubeba abiria. Imetolewa na: - Wilbrod W. Mutafugwa - DCP Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
