Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani,Khadija Nassir
amewataka wazazi wote katika wilayani Mkuranga kufanya kweli kwa kuwa na
utaratibu wa kuwafundisha watoto wao kuhusu elimu ya Hedhi salama. Nassir
ametoa rai hiyo jana wakati wa mkutano katika stendi ya Kimanzichana.
‘’Ni jukumu letu, Wazazi tuongelee Hedhi salama bila
uwoga. Takwimu zinasema mabinti wengi wanakosa masomo yao wakiwa katika kipindi
cha hedhi. Ni wakati sasa tusibaki nyuma katika suala hili’’ amesema.
Amesistiza Wazazi kutoficha kuhusu hedhi salama
kwakuwa jambo hilo bado ni changamoto kwa wilaya yake.
Katika hatua nyingine, Afisa Mtendaji wa kata ya Mkuranga,
Elizabeth Shirima amewaagiza wafanyabiashara wa soko la Mkuranga kuzingatia na
kutunza usafi wa Mazingira.
‘’Ni wakati sasa wafanyabiasahara wa soko la Mkuranga
pamoja na wakazi wa Mkuranga kutobaki nyuma katika kufanya usafi. Watu waache
uzembe na kufanya kweli katika usafi’’ amesema.
Naye Mwenyekiti wa soko la Mkuranga,Shaishi Mohamed
amesema kwa soko lao wanafanya kweli kwa kufanya usafi kila siku pia hawajabaki
nyuma katika kufanya usafi wa pamoja katika ya wafanyabiashara wa soko la
Mkuranga na stendi.
‘’Usafi ni wajibu wetu, kufanya kila siku sio mpaka
kampeni za usafi zije katika soko letu ndio tufanye usafi’’ amesema Mohamed.
.jpeg)

.jpeg)