ZAIDI WATU 2000 WAHUBIRIWA INJILI JIJINI MWANZA ,KWA SIKU MOJA,KUPITIA MAANDAMANO YA AMANI.LWC MWANZA

 

Vijana wa kanisa la living Water Centre Mwanza (Lwc),Wamefanya Uinjilisiti katika mitaa mbalimbali jijini Mwanza siku ya Jumapili ya tarehe 18.08.2024,Kupitia maandamano ya Amani.

Maandamano hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanisa hilo Bw. Furaha Musa pamoja na Katibu wake Bw. Lusungu Shani pamoja na Wachungaji wasaidizi wa kanisa hilo ambalo lina chungwa na Mtumishi wa Mungu,Mtume Onesmo Ndegi


Maandamano hayo yalianzia lilipo kanisa la lwc mitaa ya Nata Stendi karibu na Ofisi za ccm wilaya ya Nyamagana na kupita katika mitaa ya Jiji la Mwanza kuelekea katika Shule ya Kimataifa ya Isamilo,ambapo ndipo walifanya kilele cha maandamano hayo.

Waliwahubiria wananchi wa maeneo hayo zaidi ya watu waliofikiwa na Injili hiyo ni zaidi ya watu Elfu mbili (2000)


"Tulitengeneza vipeperushi elfu mbili za kuwagawia watu wote ambao tuliwafikia bahati mbaya viliwahi kuisha kutokana na Uchache wa vipeperushi hivyo,ambavyo tulitengeneza tulifikiri vingeweza kuwatosha watu,kumbe Idadi ya watu waliotamani kuvipata ilikua ni kubwa nje ya matarajio yetu' Aliongea Furaha Musa
 Bw. Furaha Musa | Mwenyekiti wa Vijana wa kanisa la living water Centre mwanza,akiwa anaongoza Maandamano ya Amani

Lusungu Shani  | Katibu wa Vijana wa kanisa la living water Centre mwanza,akiwa anaongoza Maandamano ya Amani

Maandamano hayo yalibeba Ujume wa 'ONE FOR THE LORD'LUKA 15:7 (Mlete mmoja kwa Yesu) Kama Andiko la Kitabu cha Luka 15:7 linavyosema


'NAWAAMBIA,VIVYO HIVYO KUTAKUA NA FURAHA MBINGUNI KWA AJILI YA MWENYE DHAMBI MMOJA ATUBUYE,KULIKO KWA AJILI YA WENYE HAKI TISINI NA KENDA AMBAO HAWANA HAJA YA KUTUBU'


Nje na Kuinjilisti pia walikua na mchezo mbalimbali iliyofanyikia katika shule hiyo,ni pamoja na Mashindano ya kuongelea na michezo mengine mingi pamoja Nyamba choma 

Hizi baadhi ya Picha za kwenye matukio ya Uinjilisti 


















Na Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post