Maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 406 kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto, Uhamiaji, Mgambo na Polisi wasaidizi wamejengewa uwezo kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Elimu hiyo ya kusimamia uchaguzi imetolewa leo Jumamosi Agosti 24,2024, katika viwanja vya Mabatini jijini Mwanza na Mkuu wa Mafunzo ya Polisi kutoka makao makuu ya Polisi Dodoma, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ally Lugendo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
DCP Lugendo amesema elimu hiyo ni muhimu kwa watu wote hususan askari Polisi na vyombo vingine vya usalama ili kujijengea uwezo wa kuzielewa sheria za uchaguzi ambazo kwa mwaka huu zimefanyiwa maboresho ikiwemo Sheria namba moja ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2024.
Elimu hiyo imeambatana na matembezi ya hiari (route match) pamoja na mazoezi ya viungo yenye lengo la kuweka utimamu wa mwili na ushirikiano kwa askari wa vyombo hivyo vya usalama.



.jpeg)

