"ULINZI NA USALAMA NI JUKUMU LETU SOTE", NAIBU MEYA KOTECHA

 

Naibu meya wa Jiji la Mwanza Biko Kotecha na diwani wa Kata ya Nyamagana 

Naibu meya wa Jiji la Mwanza Biko Kotecha na diwani wa Kata ya Nyamagana amewaasa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika suala la ulinzi na usalama.


Ameyasema hayo leo Agosti 21, 2024 wakati akizungumza na wafanyabiashara pamoja na wasafiri wa kivuko cha kamanga Jijini Mwanza, waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu kamishina wa Polisi DCP Wilbrod Mutafungwa, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutoa elimu na kusikiliza kero kutoka kwa wananchi wanaofanya shughuguli zao pembezoni mwa ziwa Victoria na visiwa vya mkoa wa Mwanza.


"Jukumu la ulinzi ni letu sisi sote si Jeshi la Polisi pekee, ukichukua wananchi wote wa Jiji la Mwanza kila askari awe na mtu mmoja haitawezekana lazima sisi tuwasaidie tuwe nao pamoja" ameseme KotechaNaye, Dominic Domisian dereva bodaboda wa kituo cha Kamanga Feri, ameripongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri ya operesheni ya kuzuia uhalifu hususani makosa ya usalama barabarani.


Kwa upande wake  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa amesema, amefurahi kuona imani kubwa ya wananchi kwa Jeshi lao la Polisi kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara ulio ambatana na utoaji wa elimu.


"Ni imani kubwa ambayo mnayo kwa Jeshi lenu la Polisi, tunawapongeza sana muendelee kuwa na imani hiyo ili Jeshi la Polisi ni lakwenu ambalo kazi yake ni kulinda usalama wa watu na mali zao" amesema Kamanda Mutafungwa 


Sambamba na hayo Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la urekebishaji wa kumbukumbu za mpiga kura linaloendelea, kwani Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa 


Dominic Domisian dereva bodaboda -Wakati akichangia

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post