RAIS DR MWINYI ATUA KWENYE BANDA LA BANK KUU,SABASABA DAR APEWA MAELEZO KUHUSU ELIMU YA FEDHA

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba.


Katika ziara hiyo, Dkt Mwinyi amepewa maelezo kuhusu elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu kazi za Benki Kuu ikiwemo sera za fedha, namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali, mifumo ya malipo ya taifa, na namna BoT inavyosimamia sekta ya fedha nchini.


Vilevile, Gavana Tutuba ameeleza kuhusu kazi za kitengo cha kupambana na utakasishaji fedha haramu na kazi zinazofanywa na Bodi ya Bima ya Amana.

Na mwandishi wetu kutoka Dar es salaam

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post