Mratibu wa uchaguzi Mkoa wa Mwanza Matia Levi amefafanua
kuhusu daftari la kudumu la mpiga kura ambapo amesema kuwa daftari hili ni daftari
ambalo linakuwa na takwimu mbalimbali za
wapiga kura ikiwa ni pamoja na jina mahali na eneo ambalo mtu amejiandikishia .
Ameyasema hayo kupitia kipindi cha mchakamchaka huku
akisisitiza kuwa kuanzia tarehe 21 hadi 27 kutakuwa na uandikishaji wa daftari
la kudumu la mpiga kura na baadaye kupatiwa vitambulisho kwa ajili ya uchaguzi
mkuu hapo mwakani 2025
Aidha amehitimisha kwa kutoa mwongozo wa sifa za mtu ambae
anapaswa kwenda kujiandikisha na daftari la kudumu la mpiga kura ambapo amesema
umri ni kuanzia miaka 18 na kuendelea
Zaidi kumsikiliza tumekuwekea video hapa chini bofya kumskiliza

