Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Julai, 2024 Mtaa wa Igoma kwenye Mkutano wa kusikiliza na Kutatua kero za wananchi na ndugu Matiko Migire kuwasilisha kero kwamba watumishi hao wamemuomba rushwa ya Tshs. 2,430,000 ili wafanye upimaji wa viwanja na. 311, 312 na 313 Block A Pasiansi.
Mhe. Mtanda amesema kitendo hicho si cha kiungwana na kinawanyima haki wananchi hivyo wakati TAKUKURU wanalichunguza suala hilo Idara ya ardhi amewapa siku saba kukamilisha Upimaji wa viwanja hivyo kwani wamemzungusha kwa muda mrefu mteja huyo anayefuatilia bila mafanikio.
Awali, akiwasilisha kero hiyo kwa Mkuu wa Mkoa, Matiko alifafanua kuwa 2019 Halmashauri hiyo iliomba Hati za viwanja hivyo na kuzifuta na kuahidi kufanya upimaji mwingine na kuwataka wamiliki Joseph Mashiku, Hezeline Chawachi na Desderius Ntobi kwa gharama ya 500,000 ambayo wametoa namba ya kulipia.
Ameendelea kusema kwamba Idara hiyo ya Ardhi haijawahi kutekeleza ahadi yao kwenye viwanja hivyo na badala yake wamekua wakimtafuta kwa simu kupitia mtuhumiwa Mwajuma na kumtaka atume kwenye kiasi hicho (2,430,000) ikiwa fedha halali anayotakiwa kulipia huduma ni Tshs. 500,000 tu.Akizungumzia kero ya Maji kwenye baadhi ya Mitaa ya Nyamagana, Mhe. Mtanda amesema kupitia Mkopo wenye masharti nafuu wa Tshs. Bilioni 400 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufarasa (AFD) Mamlaka ya Maji (MWAUWASA) itasambaza Maji kwenye umbali wa zaidi ya Kilomita 700 kutoka Chanzo cha Butimba na watamaliza kero kwa wananchi wengi.
Ndugu. Neli C. Msuya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA
Na mwandishi wetu kutokea Mwanza






