Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) limetoa tamko la kutowatambua viongozi wa dini wanaotumia visaidizi vya maombi kama mafuta, maji, keki, leso, chumvi na au udongo.
CPCT inayoundwa na mkanisa 12 imesema wanaofanya hivyo na vinginevyo si wanachama wao bali wanachafua Upentecoste ulioenea ulimwenguni.
Baraza hilo limetoa tamko hilo jana Ijumaa Julai 19, 2024 mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Kilele cha Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa CPCT, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji jijini Dodoma.
Tamko hilo wanalitoa kukiwa na wimbi la manabii wanao tumia visaidizi vya maombi na kulalamikiwa na baadhi wa waumini wanao tapeliwa kwa njia hiyo
Aidha katika semina hiyo ya viongozi wa CPCT, Katibu Mkuu wa baraza hilo, Dk Baraka Kihoza ametoa tamko la baraza linalojitenga na kinachoendelea viongozi wa dini wanaotumia visaidizi hivyo.
Na Mwandishi wetu kutka Dodoma