RWANDA IMEANZA KUADHIMISHA MAUAJI YA KIMBARI



Rwanda: Maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kImbari yameanza leo leo Jumapili tarehe 7 Aprili mjini Kagali.


Sherehe hizo zimeandaliwa na mwenyeji Rais Paul Kagame wa Rwanda akiandamana na mkewe Jeannette Kagame, na viongozi wengine wote wa serikali ya Rwanda.

Mauaji ya Rais wa Kihutu Juvenal Habyarimana usiku wa Aprili 6, wakati ndege yake ilipotunguliwa juu ya Kigali, yalichochea shambulio dhidi ya Watutsi kutoka kwa Wahutu wenye msimamo mkali na wanamgambo wa "Interahamwe".

Takriban watu 800,000 waliuawa, wengi wao Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Kulingana na Rwanda, mamia ya washukiwa wa mauaji ya halaiki wamesalia mafichoni ikiwa ni pamoja na katika mataifa jirani kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.

By Pascal Kadushi
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post