WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI KUFUTIWA LESENI

 

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mwl.Hassan Masala

Ziara ya Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mwalimu Hassan Masala leo Tarehe 06.03.2024 Imeendelea katika kata ya Buzuruga

Amesikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kata ya Buzuruga ambao wamejitokeza katika viwanja vya shule ya Msingi Buzuruga.

Baadhi ya kero zilizowasilishwa zimetolewa ufumbuzi hapo hapo na mkuu huyo wa wilaya moja ya kero zilizowasilishwa na Bwana Jamal,Amelalamikia bei ya sukari bado ipo juu ikiwa Mkoa wa Mwanza ulipokea Tani 250 za sukari na bado sukari wanauziwa bei ya juu.Pamoja na kutoa kero hiyo mwananchi huyo Amempongeza mkuu wa wilaya Hassan Masala kwakutoa Magari ya kutangaza  bei ya sukari kushuka bei na wauzaji kutokuuza kwa bei ya juu.

Mkuu wa Wilaya amesema watawafutia Leseni  Wafanya Biashara watakao bainika wanauza Sukari kinyume na maelekezo ya  Serikali,Pia atafikishwa mahakamani kama muhujumu wa Uchumi,Amewataka watendaji wote  kufatilia wauzaji wanaouza sukari 3500,4000,5000 mpaka 6000 ndani ya wilaya ya Ilemela na Mkoa wa mwanza kwa Ujumla

Mkuu wa wilaya ya Ilemela ametumia mkutano huo Kuwatangazia wananchi pamoja na walimuKituo cha karume kata ya bugogwa leo tarehe 06.03.2024  wamepkea wagonjwa wato (5) wa Ugonjwa wa kipindupindu,Toka wameanza kupokea wagonjwa  112 za watu ambao wamelazwa kutokana na Ugonjwa wa Kipindupindu na wameshaondolewa 

Kwa kata ya Buswelu ndani ya miezi mitatu wamepokea watu 100  ambao  Wamepitia mikononi mwa Serikali wamekua na changamoto hizo za Kipindupindu.
Amewataka walimu Licha ya kuwasaidia watoto pamoja na Walimu kuzingatia watu ambao wanafanya biashara za kuuza chakula Mashuleni kuwaratibu watu hao ni lazima wajulikane na wakaguliwe na kutambua Afya zao.

Picha Mbalimbali za matukio ya leo Kata ya Buzuruga



















Diwawani wa kata ya Buzuruga Manusula Sadiki






Post a Comment (0)
Previous Post Next Post